KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine amevunja kimya chake baada ya mkuu wa majeshi ambaye pia ni mtoto wa rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba kudai kwamba angekuwa amemkata kichwa.
Kauli ya Wine inajiri saa chache baada ya Kainerugaba kuchapisha kwenye ukurasa wa X kwamba babake, rais Museveni ndiye tu amekuwa akimsaidia Bobi Wine, bure hivyo yeye angekuwa amekata kichwa cha mwanasiasa huyo aliyekuwa msanii zamani.
“Kabobi anajua kwamba mtu pekee anayemlinda kutoka kwangu ni babangu. Kama mzee wangu hangekuwa, ningekata kichwa chake leo,” Muhoozi aliandika.
Wine kwa wasiwasi, alisema kwamba hawezi kuichukulia kauli hiyo kwa wepesi kwani ni kauli inayolenga maisha yake moja kwa moja.
Mwanasiasa huyo alidai kwamba kauli hiyo haiwezi kuwa ya utani akidai kwamba Muhoozi na babake, rais Museveni wamehusika katika mauaji ya wananchi wengine wengi tu wa Uganda.
“Tishio la mtoto wa Museveni (ambaye pia anaongoza jeshi la Uganda) la kunikata kichwa si jambo ninalolichukulia kirahisi, ikizingatiwa kwamba wengi wameuawa na yeye na baba yake, na kwa kuzingatia majaribio yao kadhaa ya kuniua. NIKATAA kutishwa na utawala waoga. Ulimwengu unatazama,” Wine alisema akinukuu chapisho hilo la Kainerugaba.
Hata hivyo, baadhi ya watu walionekana kumtetea Kainerugaba wakisema kwamba hakuwa anazungumzia Bobi Wine kwani alitumia jina ‘Kabobi’.
“"Kabobi" likawa jina lako lini. Hata Bobi Wine si jina lako bali ni jina la jukwaani. Nilidhani majina yako rasmi ni Robert Ssentamu Kyagulanyi. Ninapenda jinsi nyote mnavyoingia kwenye shambulizi la Gen MK na kwenye mhimili wake wa moto,” Charles Lepera alisema.
“Hakuna ulimwengu unaotazama kwa sababu Kabobi sio jina lako” MP Patrick Musinguzi alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!