TAKRIBANI watoto 70
wasiozidi umri wa miaka 16 walikamatwa na maafisa wa polisi wakivuta bangi
katika hafla ya karamu moja jijini Kisumu.
Kwa mujibu wa NTV Kenya, watoto hao walitiwa mbaroni mnamo Desemba 21 kaitka nyumba moja walikokuwa wamekongamana kwa karamu ya kujivinjari, tafrija ambayo ilikuwa imewavutia zaidi ya vijana 100.
NTV walibaini kwamba Kamanda wa Kaunti Ndogo ya Kisumu ya Kati Peter Mulai, alithibitisha kisa hicho akisema vijana hao walikuwa wakivuta bangi walipokamatwa.
Kamanda huyo wa kaunti ndogo alisema waliohudhuria sherehe hizo wote walikuwa watoto wenye umri wa miaka 16 na chini.
"Tuliwapata vijana hao wakiwa wameketi katika vikundi wakivuta bangi katika nyumba ambayo wamiliki wake bado hawajatambuliwa," Bw Mulai alinukuliwa na kituo hicho cha habari.
Baadhi ya watoto hao walikimbia baada ya kuruka ukuta wakati wenzao 70 walikamatwa. Walipelekwa katika kituo cha polisi cha Obung’a.
Polisi walidokezwa na jirani yake ambaye alikuwa na shauku ya kujua idadi kubwa ya vijana waliofika kwenye nyumba hiyo na muziki uliokuwa ukivuma.
Baadaye polisi walipata habari kwamba karamu hiyo ilikuwa imeandaliwa na mmoja wa vijana waliokuwa wakiishi katika nyumba hiyo.
“Tunaarifiwa kwamba watoto hao walipokea mwaliko kupitia ujumbe wa Instagram wa mwandalizi wa karamu, ambaye alidai kwamba alikuwa akitarajia zaidi ya watu 200 kuhudhuria,” asema Bw Mulai.
Sherehe hiyo
ilihudhuriwa na wavulana na wasichana kutoka shule za msingi na sekondari. Hata
hivyo, mwandalizi wa karamu hiyo anasemekana kuwa miongoni mwa watoto zaidi ya
30 walioponyoka kukamatwa kwa kuruka ukuta wa mzun
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!