MBUNGE wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewasuta baadhi ya watu katika chama cha ODM wanaoeneza kile alichokitaja kama uvumi kwamba yeye hana ushawishi kwa wananchi.


Akizungumza wikendi iliyopita, Owino alisema kwamba katika wabunge wote wa ODM, hakuna anayemzidi kwa kumfahamu vizuri kinara wa chama, Raila Odinga.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Mbunge huyo anayekisiwa kulenga wadhifa wa ugavana Nairobi katika uchaguzi mkuu ujao alionbekana kutofautiana na msimamo wa wenzake wa ODM kuunga mkono serikali ya rais Ruto, akisema kwamba japo anamheshimu Raila Odinga na misimamo yake, lakini pia ana akili zake alizokuja nazo Nairobi.


“Mimi nimekaa na mzee [Raila Odinga] sana, hakuna MP yeyote anayemjua mzee vizuri kunishinda, hakuna! Kwa sababu mimi najua ule wakati nimetumia naye Raila na yale mambo ambayo tumezungumza na yeye,” Babu Owino alisema.


“Mbona Baba mwenyewe hamjawahi msikia akisema eti hataki Babu Owino? Inatoka tu kwa watu lakini kwa Raila hutawahi sikia,” Babu Owino aliongeza.


Mbunge huyo alijipigia debe akisema kwamba yeye ni miongoni mwa watu 3 wenye umaarufu mkubwa nchini, Raila akiongoza, rais Ruto wa pili na yeye wa tatu.


“Baba tunampa heshima lakini mimi pia niko na akili yangu niliyotoka nayo Nyalenda. Kwa hivyo hayta mambo eti mtu ananibebea akili, hakuna mwenye anaweza kunibebea akili. Heshima itakuwa lakini akili yangu itabaki hivyo.”


“Lakini kama kitu ni mbaya hatutaunga mkono. Mimi mtu mwenye nilikuwa nafuata kama kichwa changu kiko chini kwa vumbi ni Baba peke yake lakini sasa kama ametoka hapo hakuna mwingine naweza fuata kama kipofu,” Owino alisema.