Wakili maarufu na seneta wa kuteuliwa Karen Njeri Nyamu amethibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi mzito sana.
Mwanasiasa huyo aliyezingirwa na utata mwingi ambaye amekuwa hospitalini katika siku chache zilizopita alithibitisha kuhusu hali yake ya uhusiano katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa Facebook.
Kutoka kwa kitanda chake hospitalini, alifichua kwamba kwa miezi saba hivi iliyopita amekuwa akichumbiana na mwanamume ambaye alimtaja kuwa mwenye upendo sana.
“Mimi si single. Sijawa single tangu Juni mwaka huu,” Karen Nyamu alisema.
Seneta huyo alifichua hayo alipokuwa akimjibu shabiki aliyedai kuwa alikuwa na mchubuko machoni, ishara ya ukatili wa kijinsia.
Nyamu hata hivyo alikanusha madai ya kupigwa na mpenzi wake akibainisha kuwa mwanamume anayechumbiana naye hawezi kumshambulia hata kidogo.
“Nina mwanaume anayenipenda sana. Huyo labda anipige busu, hawezi kunipiga. Niko na chali mtrue sana, nashukuru Mungu. Mimi si single,” alisema.
Jibu la Karen Nyamu pia lilionekana kuthibitisha kwamba sasa anachumbiana na mwanamume mwingine baada ya kudaiwa kutengana na mzazi mwenzake Samidoh.
Mwezi uliopita, Bi Nyamu alishiriki muda mzuri na mwanamume asiyefichuliwa katika uwanja wa ndege wa JKIA, kabla ya safari yake ya kuelekea mahali ambapo hapakujulikana. Alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Nyamu alionyesha sehemu ya mwanaume, huku akimshika mkono kwa kucheza naye huku akimegemea.
Aliandika "Lover girl”
Mwanasiasa huyo ambaye maisha yake yamezingirwa na drama tele alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh kwa takriban miaka minne kabla ya kudaiwa kuachana mapema mwaka huu.
Wawili hao wana watoto wawili pamoja, mvulana na msichana, ambao walipata wakati wa uhusiano wao uliojaa drama nyingi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!