
Mfanyibiashara
Sarah Njoki Nyaga almaarufu Sarah Mtalii amedokeza kwamba ndoa si rahisi, jambo
ambalo wale ambao wamekuwa kwenye ndoa wanafahamu.
Katika mahojiano ya hivi majuzi na Mungai Eve, mama huyo wa watoto wawili alidai kuwa akina mama mara nyingi hulia wakati watoto wao wanapoolewa kwa kuwa wanajua kinachowangoja.
Sarah
alisema kuwa akina mama hao hata hivyo huwa hawafichui undani wa jinsi ndoa
zilivyo ngumu kwa watoto wao kwani ni mwiko kuwaambia nini cha kutarajia.
“Unajua kwa nini unaona akina mama wakilia siku ya harusi? Hii ni kwa sababu wanajua unachojiingiza ndani yake lakini hawawezi kukuambia,” Sarah alisema.
Aliongeza, “Ni kama mwiko kuwaambia vijana mambo ya kutarajia. Huwa tunangoja muende mjionee.”
Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 45 alisema hayo alipokuwa akisisitiza ombi lake la msamaha kwa wanawake baada ya kuwashauri kuvumilia ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
Sarah alisema anaomba radhi na kueleza kuwa alisema hivyo ili kutowakatisha tamaa vijana dhidi ya kuolewa.
"Sikutaka kukukatisha tamaa wewe na mashabiki wako kwa sababu najua wewe ni wa rika moja," alimuambia Eve.
Mwanzilishi mwenza huyo wa Bonfire Adventures pia alithibitisha kuwa yuko mbioni kutengana rasmi na mumewe wa miaka mingi na mshirika wa kibiashara Simon Kabu.
Akizungumzia mipango yake inayofuata baada ya kumalizika kwa ndoa yake, alithibitisha kwamba anapanga kuolewa tena katika siku zijazo.
Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 46 alibainisha kuwa hajui jinsi ya kuwa katika uchumba kwani alilelewa kuwa mke.
“Mimi ata sijui nataka nini. Sina uhakika kama nataka
kuchumbiwa tena. Lakini ninachojua ni kwamba nataka kuolewa tena,” Sarah
alisema.
“Nimelelewa kuwa mke hivyo sijui maisha nikiwa mtaani, nikiwa single. Kwangu sijui hatua hiyo ya kuchumbiwa,” aliongeza.
Mama huyo wa watoto wawili alifichua kuwa kwa sasa yuko katika harakati za kupona kufuatia kuisha kwa ndoa yake ya miaka mingi.
"Ikiwa una mawazo ya jinsi mtu anaweza kupona kutokana na mshtuko wa moyo, ebu niambieni njia ya kupona. Mimi kwa sasa napona. Nadhani sasa ndio napata ukweli baada ya mambo kujulikana wazi,” alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!