Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya usafiri ya Bonfire Adventures Sarah Njoki Nyaga almaarufu Sarah Mtalii ameweka wazi kuwa anatarajia kuolewa tena katika siku zijazo.
Haya yanajiri baada ya habari kuibuka kuwa mfanyibiashara huyo yuko katika mchakato wa talaka na mumewe wa karibu miongo miwili na mshirika wa kibiashara, Simon Kabu.
Akizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 46 alibainisha kuwa hajui jinsi ya kuwa katika uchumba kwani alilelewa kuwa mke.
“Mimi ata sijui nataka nini. Sina uhakika kama nataka kuchumbiwa tena. Lakini ninachojua ni kwamba nataka kuolewa tena,” Sarah alisema.
“Nimelelewa kuwa mke hivyo sijui maisha nikiwa mtaani, nikiwa single. Kwangu sijui hatua hiyo ya kuchumbiwa,” aliongeza.
Mama huyo wa watoto wawili alifichua kuwa kwa sasa yuko katika harakati za kupona kufuatia kuisha kwa ndoa yake ya miaka mingi.
"Ikiwa una mawazo ya jinsi mtu anaweza kupona kutokana na mshtuko wa moyo, ebu niambieni njia ya kupona. Mimi kwa sasa napona. Nadhani sasa ndio napata ukweli baada ya mambo kujulikana wazi,” alisema.
Sarah alisema kuwa hakutaka kamwe hadithi ya mchakato wake wa talaka inayoendelea kujulikana hadharani hapo awali.
Alisema alitaka mambo kuwa siri hadi kukamilika kwa mchakato wa talaka wakati hatimaye atatoa tangazo rasmi.
"Nilitaka
hadi nitakapotangaza, niwe na cheti cha talaka," alisema.
Aidha, alibainisha kuwa licha ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika, bado anaamini katika ndoa, na yupo tayari kupa ndoa nafasi ya pili na ya tatu.
Sarah na Simon walikutana kwa mara ya kwanza kupitia kikundi cha google ambapo wote walikuwa washiriki kabla ya kukutana uso kwa uso mwaka wa 2007.
Kisha walianza kuchumbiana kabla ya Simon kumvisha pete ya uchumba mwaka wa 2008.
Wawili hao hatimaye walioana mwaka wa 2009 baada ya kujuana kwa mwaka mmoja na nusu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!