KATIBU mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchin, COTU, Francis Atwoli ni wa hivi punde kurukia kauli ya ucheshi ya ‘…hiyo kitu ikutoke’ ambayo imekuwa ikitumiwa kwa miktadha mbalimbali kwa wiki sasa.


Kupitia ukurasa wake wa X, Atwoli alitumia kauli hiyo kumjibu mtumizi mmoja wa jukwaa hilo aliyetaka kujua ni lini atastaafu kutyoka COTU.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Bwana Atwoli, utastaafu lini? Mtumizi huyo kwa jina Gideon Odinga alimuuliza.


Atwoli alisema kwamba yeye bado yuko kama mwakilishi wa vyama vya wafanyikazi nchini, akisema kwamba ni vizuri jamaa huyo ameuliza kwani swali hilo lilikuwa limemtatiza sana lakini baada ya kujikusanya kijasiri na kuuliza, limemtoka.


“Uliza tu hiyo swali hiyo kitu ikutoke…Niko hapa kuhudumia maslahi ya wanachama wa vyama vya wafanyakazi,” Atwoli alisema.


Mzee huyo ambaye amekuwa usukani kama katibu wa COTU kwa miaka kadhaa sasa alisema kwamba wadhifa wake hakuteuliwa bali yeye huwa anachaguliwa na wanachama huku akifafanua kwamba watu wengi hawawezi elewa jinsi vyama vya wafanyikazi hufanya kazi hadi pale watakapokuwa wanachama.


‘Sijateuliwa, nachaguliwa na wanachama. Ukijiunga na muungano, utaelewa jukumu langu na la COTU (K),’ Atwoli aliongeza.


Taaluma yake ilichukua mkondo wa kimataifa alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa COTU yenye nguvu mwaka 2001, nafasi ambayo amechaguliwa kwa mihula mitano mfululizo.


Uchaguzi wa hivi punde ulifanyika katika Chuo cha Wafanyakazi cha Tom Mboya huko Kisumu, ambapo mamia ya makatibu wakuu wa muungano wa COTU walihudhuria, na angalau wengine 200 walihudhuria kwa njia ya mtandao.


Katika hotuba yake ya kukubali kuchaguliwa tena, Katibu Mkuu wa COTU (K) Francis Atwoli aliwashukuru wajumbe na wafanyikazi wa Kenya kwa ujumla kwa kumwamini na majukumu mengine. Aliahidi kamwe hatasaliti imani ambayo wafanyikazi wote wamempa kwa miaka iliyopita.