DHEEBU la PEFA limeonekana kuenda kinyume na
madhehebu mengine mengi humu nchini kuhusiana na suala la kupokea na kurejesha
sadaka na matroleo yote yanayoletwa na wanasiasa.
Katika mkutano na waandishi wa Habari, mchungaji wa PEFA alisisitiza kwamba kanisa hilo haliwezi kukataa kupokea sadaka kutoka kwa wanasiasa kwa sababu hawawezi kujua sadaka hizo kama ni mafao ya ufisadi au la.
Msimamo wao unajiri wiki moja tu baada ya muungano wa makanisa nchini NCCK kupitisha kwa kauli moja kutokubali sadaka kutoka kwa wanasiasa na pia kurejesha zile ambazo zimeshapokelewa.
Kanisa hilo limesema kuwa litaendelea kufanya kazi na tabaka la kisiasa, kuwakaribisha wanasiasa katika matawi yake 3,000 kote nchini.
“Kuna madhehebu ambao wamesema kwamba sadaka watakuwa wanaangalia, kunai le watakuwa wanakubali, kuna ile watakataa lakini sisi kama ushirika wa PEFA bado hatuna mbinu ya kukagua ni gani inakubalika na ni gani inakataliwa. Kwa hivyo kuanzia sasa hivi kuendelea mbele bado tutazipokea sadaka zote na tutaziweka katika kazi,” mchungaji aliambia waandishi wa habari.
“Sisi kama PEFA haturudishi sadaka, kwa sababu hatuwezi kujua hizi sadaka zimetoka wapi unless tuwe na mikakati ya kuziangalia. Tunashukuru wote ila tunasema sadaka ikitolewa isitangazwe,” aliongeza.
Hii ni licha ya upinzani wa umma ambao makanisa ya Kikristo yamepokea kuhusu hili. Wakenya wengi wamedai kuwa michango hiyo inaibua masuala ya kimaadili ambayo yanaweza kuchafua taswira ya Kanisa nchini Kenya.
Msimamo wao unakuja huku makanisa ya Kikatoliki na Kianglikana yakitoa maagizo kwa makanisa yao kusitisha kuchukua michango ya pesa kutoka kwa wanasiasa na kuelekeza matawi mahususi kurejesha michango ya kisiasa.
Mjadala kuhusu michango ya kisiasa makanisani ulianza Novemba 19, wakati Kanisa Katoliki lilipoelekeza makasisi katika Kanisa Katoliki la Soweto kurejesha Ksh5.8 milioni kutoka kwa Rais William Ruto.
Rais Ruto alitoa Ksh 600,000 kwa Kanisa Katoliki la Soweto jijini Nairobi kwa wanakwaya na Ksh2 milioni ambazo zingetumika kujenga nyumba ya baba.
Pia aliahidi kuchangia Ksh3 milioni za ziada ambazo zitatumwa kwa akaunti ya kanisa kununua basi la kanisa. Wakati wa hafla hiyo, Gavana Sakaja alitoa Ksh200,000 kwa kanisa moja
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!