MSHTAKIWA anayetuhumiwa kwa kcuhapisha ujumbe wa
uongo kuhusu rais William Ruto katika mtandao wa kijamii ametoa ombi kwa
mahakama kumwasilisha rais mahakamani.
Mwanafunzi huyo wa chuo kikuu alifikishwa mahakamani Jumatano kwa shtaka la kumshushia rais kifo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii.
David Ooga Mokaya ameitaka mahakama kuamrisha DPP Renson Ingonga kumpa nakala za mashahidi, ikiwemo ile ya mlalamikaji ambaye alisema ni rais Ruto mwenyewe.
Chama cha mawakili nchini, LSK ambacho ndicho kinaongoza upande wa utetezi kinasema kwamba ni sahihi kwa DPP kuangalia upya kesi hiyo wakiitaja kama kesi isiyo na maslahi ya umma.
Mwanafunzi huyo wa mwaka wa 4 katika chuo kikuu cha Moi alifika katika mahakama ya Milimani akiwa ameandamana na mawakili wake Danstan Omari na Ian Mutiso.
“Tungependa kumuoa rais, mheshimiwa Ruto kufika mahakamani na kutoa ushahidi kwamba ako hai na si yeye alikuwa katika lile jeneza. Hiyo itakuwa ni aibu ya kitaifa, kwa sababu tutakuwa tunataka kwamba afike mahakamani kutoa ushahidi,” alisema Danstan Omari.
Mawakili hao waliitaka mahakama kuamuru mteja wao ambaye anasburi kufuzu Desemba hii kutoka chuoni kurudishiwa vifaa vyake vya kiditali kama simu.
Mawakili hao walisema kwamba kesi hiyo haina mashiko yoyote na kwamba watamwandikia DPP Barua ya kutaka kufutiliwa mbali kwani mteja wao si wa kwanza kumshtumu rais Ruto mitandaoni.
‘Tuliona kwenye mitandao ya kijamii mtu akifikishwa mahakamani kwa kufoka ‘Ruto sharti aende’. Na mahakama ilifutiliwa mbali shtaka hilo ikisema hakuna mashtaka. Ningependa kusema kwamba waache Wakenya wafurahie uhuru wao wa kuzungumza na kwa ubunifu. Acha ofisi ya ODPP isimame kidete na kusimamisha DCI kutoka kwa kuaibisha ofisi yake,” wakili Omari aliongeza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!