RAIS William Ruto ametania kwamba nchini Kenya kuna pepo chafu ambayo ni ya kuleta upingamizi katika kila hatua serikali inanuia kufanya.


Akizungumza katika kaunti ya Taita Taveta wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kusambaza madini ya chuma cha Devki, alisema kwamba kuna baadhi ya makundi ya Wakenya ambao wameshambuliwa na pepo hiyo ambayo wanaona fursa ya kupinga kila kitu serikali inafanya.


Kiongozi wa taifa alipiga hatua na kuorodhesha baadhi ya miradi ya serikali ambayo Wakenya Fulani wamekuwa wakipinga.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


“Mimi nataka niwaulize Wakenya, tafadhalini, kuna pepo chafu ya upingsmizi, kupinga kila kitu. Kiwanda kama hiki, watu wanapinga, ujenzi wa nyumba za bei nafuu wanapinga, chanjo ya ng’ombe kuondoa magonjwa, wanaipinga, kubadilisha mfumo ndio tuweze kuokoa vyuo vyetu ambavyo vilikuwa vinakwama wanapinga…”


“Wanapinga hata miradi yoyote ya serikali. Mambo ya bima ya afya kwa wote wanaipinga, mambo ya afya wanapinga. Sasa mimi  nauliza, hii pepo chafu nafikiri hata imefikia hatua wanapinga hata matoleo kanisani,” Ruto alisema huku hadhira ikicheka.


Ruto alisema kuwa pepo hiyo ya kupinga kila kitu inahitaji maombi kwa taifa, akiwarai wananchi kuombea nchi.


“Hii pepo ya kupinga kila kitu, tuombee nchi yetu. Ama niaje jamani? Hivyo wale wanapinga kila kitu sijui mitandaoni, sijui wapi tunawaambia shetani ashindwe,” Ruto alikariri.



Akionekana kurejelea dili aliyositisha ya upanuzi wa JKIA ambayo ilinuiwa kuchukuliwa na kampuni ya Adani, rais alisema kuwa wale waliokuwa wanapinga dili hiyo wengine wao hata hawajawahi fika katika uwanja wa ndege.


“Niliona hata watu wengine kufurahia eti upanuzi wa uwanja wa ndege umeghairishwa. Eti sasa wale wamesitisha ujenzi wa airport ni mashujaa. Mashujaa wa kufanya kitu gani? Airport pale iko kwa runway, inavuja iko kwa turubai, nchi zingine wanajenga airport zao na sisi yetu hapa Kenya sijui ni ya aina gani. Halafu kuna watu wanaongea hapo eti tumeshinda sababu tumesimamisha kujenga airport.”


“Ni faida gani unapata wakati unasimamisha ujenzi wa uwanja wa ndege katika nchi yako? Na huna mpangp mbadala jinsi ya kujenga airport mpya. Wale wanapinga hata hawajawahi kukanyaga kwa airport hata siku moja,” Ruto alifoka.