MJUZI wa masuala ya kisiasa, Mutahi Ngunyi ametoa rai ya pekee kwa rais William Ruto kumteua aliyekuwa waziri wa afya katika serikali ya Uhuru Kenyatta, Mutahi Kagwe kama waziri katika wizara hiyo.


Kupitia ukurasa wake wa X, Ngunyi alitoa maoni kwamba Kagwe ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya kwenye bima ya SHA ili kuongeza Imani ya wananchi katika bima hiyo ambayo imezua hoja nyingi tangu kuzinduliwa miezi miwili iliyopita.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ushauri wake unajiri wakati ambapo inasemekana kuwa rais Ruto anatarajiwa kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baadae wiki hii.


Ruto anatarajiwa kutangaza mabadilizo katika wizara mbalimbali, huku pia akitarajiwa kumteua waziri wa kuchukua wizara ya usalama wa ndani iliyoachwa wazi baada ya Kithure Kindiki kuteuliwa kama naibu wa rais.


Ngunyi alimtahadharisha Ruto dhidi ya kuiweka wizara ya usalama wa ndani mikononi mwa watu wasio wanachama wa UDA, akisema kuwa wizara hiyo itakuwa muhimu katika kuchaguliwa kwake tena kama rais, 2027.


“Mpendwa Ruto: Mwanamume UNAYEMCHAGUA kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani atakuwa CHANZO CHA KLUCHAGULIWA KWAKO TENA 2027. Ninajua hili kutoka kwa EXPERIENCE. LAZIMA uchague INSIDER kutoka UDA. Si INCHI zaidi; Sio chini ya INCHI. Mpe mtu wa Uhuru Afya. Iwapo ALIREKEBISHA COVID, anaweza kurekebisha SHA na SHIF,” Ngunyi alishauri.


Ushauri wake kwa rais dhidi ya kutomteua mtu asiye mwanachama wa UDA kwenye wizara ya usalama wa ndani unajiri wakati kuna sekeseke kwamba kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa ambaye ni mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohamed ni miongoni mwa wale wanaopigiwa upato kurithi Kindiki kwenye wizara hiyo.


Kindiki aliapishwa mwezi mmoja uliopita kama naibu rais, baada ya kumalizika kwa mchakato wa kubanduliwa ofisini kwa aliyekuwa naibu rais, Rigathi Gachagua.


Baada ya kuapishwa kwake, majukumu ya wizara ya usalama wa ndani yalitwikwa waziri mwenye mamlaka makuu, Musalia Mudavavi ambaye mpaka sasa anashikilia ofisini hiyo kikaimu.


Kagwe alijizolea umaarufu haswa kipindi cha covid-19 mwaka wa 2020 ambapo alijibiisha kuwataarifu wananchi kuhusu maendeleo ya janga hilo.