KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Novemba 26.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Nyeri, na Homabay.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Tassia na Pipeline zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Karia, Gitero, na Kigogoini katika kaunti ya Nyeri yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za Kandiege na Kanyamfwa katika kaunti ya Homabay pia zitakisa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!