KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Novemba 24. 

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na West Pokot, Siaya, na Kiambu.

Katika kaunti ya West Pokot, maeneo ya Ortum, Sigor na Sina yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Shianda na Ragegni katika kaunti ya Siaya yataathirika kati ya saa mbili na nusu asubuhi na saa kumi na moja unusu jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baadhi ya sehemu za Kiambu Road na Karia katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya sa sita adhuhuri na saa nane mchana.