
MWANAMKE mmoja aliyekuwa
mjamzito amefariki baada ya kutokwa damu kupita kiasi wakati wa jaribio la
kumkeketa lililoenda mvange katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Mwanamke huyo
aliripotiwa kufa mikononi mwa wanawake wenza ambao walijukumiwa na shughuli ya kumfanyia kitendo hichi
kilichopitwa na wakati.
Wake wenza hao
walifanyiwa ukeketaji ulioharamishwa katika eneo la Kocholwo, kaunti ndogo ya
Keiyo Kusini alfajiri ya Jumanne lakini iligeuka msiba baada ya mama mdogo
kufariki kutokana na kuvuja damu nyingi.
Mwanamke mkubwa
alikimbizwa katika hospitali ya karibu. Kulingana na mamlaka, wake wenzi hao
wanaweza kuwa walilazimishwa na waume zao kumfanyia unyama huo.
Siku ya Jumatano, polisi
walikuwa bado wanamfuatilia mwanamume huyo mwenye wake wengi ambaye inasemekana
alitoroka baada ya mke mdogo kufariki.
Naibu Kamishna wa Kaunti
ya Keiyo Kusini, Diana Wekesa jana aliambia vyombo vya habari kwamba uchunguzi
wa awali unaonyesha mumewe alipanga tohara hiyo.
Bi Wekesa alisema tohara
ilifanywa kisiri nyumbani kwa mwanamume huyo. Mke wa marehemu, kulingana na
maafisa wa polisi wanaochunguza kisa hicho, alikuwa na umri wa miaka 26 huku
mke mkubwa akiwa na umri wa miaka 40.
Bi Wekesa alisema polisi
walikuwa wakimhoji mwanamke mwenye umri wa miaka 70 anayeshukiwa kutekeleza
kitendo hicho.
“Tahadhari ilitolewa
Jumanne mchana kwamba mwanamke ambaye alikuwa amekeketwa alikuwa ametokwa na
damu nyingi. Chifu msaidizi wa eneo hilo alikimbia hadi eneo la tukio ambako
ndiko nyumbani kwa wake wenzake na kugundua kuwa mke mdogo alikuwa tayari
amefariki,” alisema jana.
Alisema ziara ya mamlaka
katika nyumba ambayo tohara ilifanywa iliripoti kuwa eneo lilikuwa limejaa
damu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!