Kisa cgha kuskitisha ambacho kimevutia hisia mseto mtandaoni kimeonyesha watoto wawili wavulana wakiadhibiwa vikali barabarani huku wakicheza densi.

Katika klipu hiyo fupi iliyochapiwa kwenye ukurasa mmoja wa TikTok, wavulana hao walionekana wakishushiwa kichapo huku wakicheza densi katika kile kilichoonekana kama ni kushurutishwa.

Inaarifiwa kwamba vijana hao waliiba simu aina ya iPhone 14 pro-max yenye tamani ya zaidi ya laki mbili pesa za Kenya.

Kisha waliipiga mnada kwa takribani shilingi elfu 8 tu pesa za Kenya, kwa kutojua thamani yake halisi, jambo ambalo liliwakasirisha watu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kukamatwa na kukiri kuiba na kuuza simu hiyo, maskini vijana wa watu walishushiwa kichapo kikali huku wakitakiwa kucheza densi.

Kichapo kilionekana kuwa kama kichocheo cha densi yao huku wapiti njia wakiwarekodi kwa mbwembwe na madoido.

Video hiyo ilizua maoni baadhi wakiwahurumia vijana hao na wengine wakiunga mkono adhjabu hiyo kwa kauli kwamba ni vizuri kumkunja kambare angali mbichi.