Mtayarishaji maudhui maarufu, Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy, ​​ametoa tahadhari kwa wanawake  ambao wanafikiria kuzaa.

Katika chapisho la Alhamisi asubuhi, mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Stevo Simple Boy aliwashauri wanawake dhidi ya kuzaa kwa ajili ya wanaume.

Vishy alionya kuwa wanawake wanaozaa kwa ajili ya wanaume wako katika hatari ya kuwa mama single.

"Wakati wowote uko tayari kupata ujauzito kwa ajili mwanaume, pia uwe tayari kuwa mama asiye na mwenzi hivi karibuni," Pritty Vishy alisema.

Aliongeza, "Wanawake wanapaswa kuzoea kuzaa kwa ajili yao wenyewe sio kwa ajili ya mwanaume."

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mtayarishaji huyo wa maudhui pia alitaka wanawake kuhakikisha kwamba wapenzi wao pia wako tayari kuwa wazazi kabla ya kukubali kuwazaa.

"Kabla ya kupata mtoto na mwanamume lazima umuulize mara kwa mara ikiwa anataka kuwa baba. Pia usikimbilie, inachukua muda kujua ikiwa anapenda watoto, "alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa Stevo kwa sasa ana umri wa miaka 23 na hana mtoto yeyote. Yeye pia hayuko katika uhusiano wowote unaojulikana.