Mwili wa shemeji wa aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta unatazamiwa kuzikwa jijini Nairobi siku ya Jumanne.

Familia ya Kenyatta imekuwa katika majonzi kufuatia kifo cha shemeji wa Uhuru William Gakuo.

Gakuo, ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 48, ni kakake aliyekuwa Mkewe Rais Margaret Kenyatta.

Alikufa Jumatano, Novemba 6 nyumbani kwake Karen.

Polisi walisema Gakuo alifariki kwa kujitoa uhai.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mkewe, Sheila, aliripoti kwamba Gakuo alipatikana akining'inia kwenye korido inayoelekea chumbani kwake na kwamba alikuwa na barua ya kujitoa uhai karibu naye.

Suala hilo linasubiri kuchunguzwa.

Kulingana na taarifa ya familia, marehemu amemwacha mke, Sheila Wanjiku Mwangi.

"Ni kwa huzuni kubwa na kukubali kwa unyenyekevu mapenzi ya Mungu kwamba tunatangaza kufariki kwa William...Ndugu ya Gabriela, Maina, Christine na Margaret," ilisoma taarifa hiyo.

Mwili wa Gakuo utachomwa mnamo Novemba 12 katika eneo la Hindu Crematorium, eneo la Kariokor, Nairobi.

Akiwa na asili yake katika eneo bunge la Kangema kaunti ya Murang’a, marehemu alizaliwa na Dkt Ephantus Njuguna Gakuo, mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Reli la Kenya, na mama Mjerumani Magdalena Njuguna.

Dkt Njuguna alikua mkurugenzi mkuu wa kwanza Mwafrika wa Shirika la Reli la Kenya baada ya kuchukua wadhifa wa GPG Mackay mnamo 1964, mwaka ambao Mama Margaret alizaliwa.

Alichukua shirika hilo baada ya kurejea kutoka Ujerumani ambako alikuwa amefundisha kwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu PhD katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Freiberg.

Dkt Njuguna alishikilia wadhifa huu kwa miaka 12 na kuondoka mnamo 1976 William alipozaliwa.

Aliaga dunia mwaka wa 2005. Ripoti zinaonyesha kuwa alichangia Uhuru kukutana na Margaret, na kusababisha uhusiano uliofikia kilele cha ndoa na kubarikiwa kupata watoto.