Rapa anayejinadi kama nambari moja wa Kenya kwa muda wote, Khaligraph Jones amedokeza kuwa ujenzi wa jumba lake la kifahari ambazo limezua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii huenda ulichochewa na maisha ya kifahari ya rapa kutoka Marekani, Rick Ross.

Jones alichapisha video kwenye Instagram yake akionyesha ukubwa, upana na umaridadi wa jumba hilo na kusema kwamba wengi wa watu ambao wanakejeli muundo na ujenzi huo ni wale ambao hawajazea kuona mijengo ya kibinafsi kama hiyo.

Msanii huyo alisema kuwa kwa jinsi ameboresha mazingira ya jumba hilo la kifahari, watu wanaokwenda kule watapata kuhisi uwepo kama ule wa boma la Rick Ross.

“Hamjazoea hizi settings, hapa ukikuja ni kama umeingia Amerika, kwa Rick Ross. Heshima ni lazima kwa OG,” Khaligraph Jones alisema huku akicheka.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Siku ya Jumatatu, Jones alishangazwa na watu ambao walikuwa wanachapisha picha na video za jumba lake mitandaoni wakiambatanisha na kauli za dharau kuhusu mjengo huo.

Hata hivyo, alionyesha kutoshtushwa na kauli hizo hasi akisema kwamba habari za kusemwa kuhusu mafanikio yake ndizo habari ambazo alikuwa akiomba kwa muda mrefu.

"Unaamka unapata unatrend sababu umejenga nyumba kubwa inakaa kama maduka, Mungu anajua haya ndio matatizo niliyokuwa natamani," Khaligraph alisema.

Jones amekuwa akionyesha maendeleo ya ujenzi wa jumba hilo ambalo liko viungani mwa Ngong tangu lilipoanza.

Wengi wamekuwa wakimsuta kwa ujenzi huo wanaoufananisha kama duka la jumla, wengine wakiutaja kama mjengo wenye mfanano wa chuo kikuu, lakini yeye amesimamia kauli yake kwamba ni boma lake la kuishi wala si la kufanya biashara.