Chuo kikuu cha Moi chawasimamisha kazi maafisa wa UASU kutokana na mgomo Chuo kikuu cha Moi kimewasimamisha kazi maafisa wa UASU kutokana na mgomo unaoendelea ambao umelemaza masomo kwa muda wa miezi miwili iliyopita.
Maafisa wa muungano huo pia wamezuiwa kuingia chuoni humo na kufungiwa nje ya lango kuu la chuo hicho. Viongozi hao wakiongozwa na katibu wa UASU tawi la chuo hicho Ojuki Nyabuta walithibitisha kupokea barua za kusimamishwa kazi zilizotiwa saini na Makamu Naibu Chansela wa Usimamizi Profesa Kirimi Kiriamiti.
"Tumepokea barua za kusimamishwa kazi na tumezuiwa kuingia katika chuo hicho kikuu," alisema Ojuki. Alisema wamelazimika kufanya mkutano nje ya lango la chuo kufuatia hatua hiyo ya uongozi wa chuo hicho.
"Hatutatishwa na tunasalia kwenye mgomo hadi tulipwe malimbikizi yetu ya mishahara," Ojuki alisema.
Alisema pia walipokea barua za kuwataka wahadhairi zaidi ya 1,000 kuleza sababu ya kshiriki mgono. Chuo kikuu cha Moi kilifunguliwa tena wiki iliyopita na wanafunzi wameripoti lakini masomo bado yamelemazwa.
UASU ilikataa kuhudhuria mikutano na wasimamizi wa Chuo Kikuu cha Moi katika majaribio ya hivi punde ya kumaliza mgomo huo. Juhudi za wasimamizi wa Chuo Kikuu cha Moi kuafikia makubaliano ya kurejea kazini na wafanyikazi waliogoma zilikosa kuzaa matunda.
Naibu Chansela Profesa Isaac Kosgey alikuwa ametoa waraka unaoelekeza kwamba masomo yarejee chuoni Jumatatu, Novemba 11, 2024, lakini Muungano wa Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu (UASU) ulitangaza kwamba wanachama wake walisalia kwenye mgomo hadi walipwe marupurupu yote ya mishahara.
Ojuki alisema majaribio ya kuwa na mkutano wa kusuluhisha mgomo huo yaliporomoka kwa sababu wasimamizi wakiongozwa na Kosgey walialika muungano huo kwa mazungumzo Jumamosi na Jumapili lakini ni baraza pekee lililopewa mamlaka kufanya hivyo.
“Uongozi sio mwajiri wetu. Sheria inasema tumeajiriwa na halmashauri ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kujadiliana nasi na hivyo haikuweza kuhudhuria vikao visivyo halali na menejimenti. Ojuki.
Kamati ya bunge ya ilikuwa imeagiza uongozi wa chuo hicho kuafikia makubaliano ya kurejea kazini mara moja na wafanyikazi lakini UASU ilisema agizo hilo halitekelezeki kwa sababu mgomo ni mchakato ambao hauwezi kutatuliwa kwa urahisi.
"Tuko hapa kuelewa hali halisi na kuangalia njia ambazo tunaweza kusaidia kufanya chuo kikuu kuanza tena hali ya kawaida," alisema Melly.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!