Mwanamume mmoja amejipata katika njia panda baada ya mke wake kumshauri kufanya mapenzi na bosi wake wa kike ili kupata mkataba wa kudumu kama mfanyikazi.


Mwanamume huyo ambaye jina lake lilibanwa alituma ujumbe fiche kwa mshawishi mmoja wa mtandaoni akiomba ushauri kuhusu hilo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Alieleza kwamba alijipata chini ya shinikizo baada ya bosi wake wa kike aliyempa kazi ya mkataba wa miezi 3 kumtaka kufanya mapenzi naye ili kumwajiri kwa mkataba wa kudumu.


“Mimi ni mwanamume aliyeoa mwenye umri wa miaka 37. Nilipoteza kazi yangu mwaka wa 2021 na tangu wakati huo nimekuwa nikihangaika kupata kazi. Julai nilipata kazi lakini ni mkataba wa miezi mitatu. Bosi wangu ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36. Aliniambia nikimpa mtoto atanipa nafasi ya kudumu,” mwanamume huyo alieleza.


Baada ya pendekezo la bosi, jamaa huyo ambaye alikiri ni mchamungu nambari moja, alimuelezea mkewe akitaka kupata ushauri.


Cha ajabu, mkewe alimshauri kukubali pendekezo la bosi wake kwa ajili ya kupata riziki ya kudumu, jambo ambalo lilimuacha mwanamume huyo katika njia panda.


Alisema kwamba mkewe alimgombeza akimwambia ni visingizio vya kutotaka kufanya kazi alikuwa anatafuta, na kumtaka kurudi kwa bosi wake upesi na kumwambia amekubaliana na wazo lake.


“Nikiwa Mkristo, nilikataa na kumwambia mke wangu. Mke wangu alikasirika na kunishutumu kuwa sitaki kufanya kazi. Sasa ananilazimisha nirudi kwa huyo mwanamke na kumwambia nitafanya. Mimi ni Mkristo na niliweka nadhiri mbele za Mungu kwamba nitakuwa mwaminifu kwa mke wangu. Sasa yeye ndiye ananilazimisha kutokuwa mwaminifu,” alieleza zaidi.


Jamaa huyo aliomba ushauri jinsi ya kusuluhisha hilo, akisema kwamba mkewe ndiye amekuwa akifanya kazi za ziada ili kukidhi mahitaji ya familia wakati wote tangu alipopoteza kazi mwaka 2021.


Amekuwa akifanya kazi mbili kwa miaka miwili iliyopita ili kunitunza mimi na watoto. Ninaelewa kuwa mambo ni magumu, lakini je, ni lazima nitende dhambi ili nipate mshahara? Vipi kuhusu wow wetu?" alitaka kushauriwa.


Je, ungependa kumshauri jamaa huyu vipi?