Rapa kutoka Tanzania Billnass ambaye ni mume wa Nandy amemmwagia sifa kemkem malkia huyo wa bongofleva kwa upendo na sifa wakati akisherehekea miaka 32 ya kuzaliwa kwake.

Mumewe Nandy alimfanyia sherehe ya faragha ya siku ya kuzaliwa ya mialiko pekee ambayo ilikuwa na mandhari nyekundu na nyeusi. Pia alizama kwenye mitandao ya kijamii kummiminia sifa tele, akimtaja kama mwanamke mwenye akili na uzuri.

"Katika Sala Na Duwa ambayo Kila Siku Nikiamka Huwa Nakumbuka Kumshukuru Mungu na Kusema Ahsante…Ni Kukufanya Wewe Kuwa Sehem ya Maisha Yangu…Nakiri ya Kuwa Mwenyezi Mungu amenipendelea sana Kwa Kunipa Mwanamke Mzuri, Mwenye Akili, Hekima, Busara, Upendo, Umenizalia Mtoto Mzuri. na Umetenga Muda wa Kumlea Vyema, Unanipa Furaha kila iitwapo leo kwa kunipa Faraja Maneno Mazuri Na Maono…"

Aliongeza"Natamani Sana Ulimwengu Mzima Ujuwe Namna Ninavyokupenda…Kwa Bahati Mbaya Mm Sio Mzuri sana Kwenye Kuandika na Hayo ni Machache nisaidie Kusema Mengine nitaandika Kwenye Kitabu chetu cha Mapenzi yaliyojaa Furaha…Chenye kutanabaisha Mazuri Yako Mengi…Heri ya Siku ya Kuzaliwa My Everything, My PYG… , Rafiki Yangu a k a Kenaya's Mama"

Wanandoa hao wamebarikiwa mtoto mmoja pamoja.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans