Mchekeshaji na muigizaji kutoka Mwihoko Ithagu Kibicho almaarufu Henry Desagu yuko sawa na mwenye afya njema, licha ya wasiwasi wa awali kuhusu hali yake.

Siku ya Jumamosi, Novemba 9, msanii huyo mcheshi alitoa taarifa ya video kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii akionyesha kuwa anaendelea vizuri. 

Mtumbuizaji huyo ambaye siku chache zilizopita alizua wasiwasi miongoni mwa Wakenya alikuwa pamoja na marafiki watatu ambao pia walithibitisha kuwa yuko vizuri.

“Timu Mwihoko, timu umbwedede, tunasema mambo iko best. King of Mwihoko mwenyewe ako hapa, ako ngangari,” Desagu alisema kwenye video hiyo.

Rafikiye aliyekuwa akirekodi video hiyo alipuuzilia mbali madai kuwa alikuwa katika hali mbaya na kuwataka Wakenya kukoma kueneza madai ambayo hayajathibitishwa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Aliwataka mashabiki kuepuka kuchafua majina ya watu wengine akisema kuwa haisaidii.

“Tulieni, sijui unataka aje mtu ukichafulia mwenzako jina ama ukiongea vitu sijui zinakaa aje kusema kweli. Kila mtu hapa anajaribu kujilea. Uchumi ni ngumu bana, sasa unaongelea mtu sijui unasema vitu gani, rafiki yangu watu wanapitia mambo sasa wewe unafanya mambo kuwa ngumu zaidi na kuharibia maisha ukiongea vitu hujui. Sasa si ndiye huyu basi, ndo huyu ako sawa, ako chonjo,” alisema.

Desagu ambaye alionekana kuwa na furaha na kusisimka katika video hiyo alithibitisha kuwa kila kitu kiko sawa na kuwatakia kila mtu wikendi njema.

"Mimi sina ngori yoyote," alisema.

Mapema wiki hii, ripoti ziliibuka kuwa mchekeshaji Desagu aliokolewa na Wakenya wa nia njema akiwa katika hali iliyodaiwa kuwa ya huzuni.

Madai kuwa mtumbuizaji huyo hakuwa sawa yalitolewa kwenye mtandao wa Facebook na kuungwa mkono na mwanamuziki wa Kikuyu Karangu Muraya.

Mtumiaji wa Facebook Mwalimu Francis Njiriri aliandika;

“Marafiki naomba tujifunze kuwachunguza walio katika mduara wetu.Nilikutana na post ya jana ya Henry Desagu ambapo alitaja kujisikia si salama na huenda wengi waliipuuza kuwa ni post nyingine ya kimaudhui. Hata hivyo baadaye alifafanua. kwamba alikuwa salama.

Asubuhi ya leo mwendo wa saa 9:40 asubuhi, nikiwa katika harakati za kuzunguka Barabara ya Thika-Ngoingwa-Mangu, nilishuhudia tukio la kutatanisha. Kijana mmoja alikuwa akitembea katikati ya barabara akionekana kutokusumbua huku magari yakimpigia honi. Nashukuru, kwa neema ya Mungu, niliamua kushuka kwenye gari langu na kuangalia hali ilivyo. Kwa usaidizi wa watu wachache wenye mioyo ya fadhili, tuliweza kumkaribia—na ikawa Henry Desagu,” alisema.

Aliongeza;"Hakuwa na akili timamu, akipiga kelele na kuzungumza bila kusita. Bila kusita, nilimsaidia ndani ya gari langu na, pamoja na wengine, tukamkimbiza Hospitali ya Level 5. Huko, daktari wa akili mwenye huruma, Dk Catherine, alimhudumia. Asante sana kwa kila mtu ambaye alipitia wakati nilipofikia - Mungu awabariki nyote"