Kuna majimbo 50 nchini Marekani na mengi yao hupigia kura chama kimoja katika kila uchaguzi.

Lakini kuna majimbo machache - yanayojulikana kama majimbo muhimu - ambapo mgombea yeyote anaweza kushinda.

Majimbo haya ni Nevada, Arizona, North Carolina, Georgia, Wisconsin, Michigan na Pennsylvania.

Majimbo yenye watu wengi ndio muhimu zaidi, ikitafsiriwa kwa idadi ya kura 270 za wawakilishi maalum wanaomchagua rais zinazohitajika chini ya mfumo wa kura za majimbo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kuna kura 538 za wawakilishi hao ambazo mgombea anaweza kujinyakulia kwa jumla.

Rais ajaye atakuwa mgombea atakayepata kura 270 au zaidi za wawakilishi hao maalum.

Wagombea wote wawili watahitajika kushinda angalau majimbo matatu muhimu ili kuwapitisha kwenye idadi ya kura ambazo ni lazima kupata.

Trump ashinda katika jimbo la Florida huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea



Shangwe na nderemo zimetawala upande wa Donald Trump huko Palm Beach, Florida alipotangazwa kuwa anayetarajiwa kupata ushindi katika jimbo hilo.

Haikuwa na shaka kamwe kwamba angeweza kupata ushindi katika jimbo hilo ambalo kwa sasa Republican ndio wako kifua mbele.

Kulingana na mchambuzi wa BBC, Anthony Zurcher, siku za jimbo la Florida kuwa uwanja wa kutafuta ushindi wa urais zimepitwa na wakati.

Miaka 24 iliyopita, kura mia chache katika jimbo hilo zilikuwa kichocheo cha kupata urais kwa George W Bush wa chama cha Republican dhidi ya Al Gore wa Democrat.

Kwa sasa, 73% ya kura zikiwa zimehesabiwa, Donald Trump amekadiriwa kushinda jimbo hilo.