Mahakama moja katika jiji kuu la Nigeria, Abuja imempa adhabu ya kuosha choo kijana mmoja aliyeshindwa kulipa ada ya huduma ya kunyolewa kwenye kinyozi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alijipata kizimbani baada ya kukosa kulipia huduma ya kunyolewa.

Kijana huyo alinyolewa na kinyozi akamwambai huduma ilikuwa inamgharimu Ksh 2,000 ambazo alikosa kulipa kupelekea kesi yao kuhamia mahakamani.

Baada ya ushahidi wote kuwasilishwa mahakamani, alipatikana na hatia ya kutolipia huduma ya kunyolewa na hakimu kumpa adhabu ya kuosha vyoo vya hospitali kwa siku 10. Aliiomba mahakama imsamehe na kuongeza kuwa halitafanyika tena.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hakimu Mwandamizi aliamuru maafisa wa masahihisho wasimamie ili kuhakikisha kwamba anamaliza kifungo.

Alimuonya kuacha kufanya uhalifu. “mshtakiwa alikwenda kwenye saluni ya kunyoa nywele ya mlalamishi ili kukata nywele na baada ya kunyoa nywele, alikataa kulipa ₦ 27,000 kwa huduma hizo,” kiliripoti chanzo kimoja.