Misukosuko ya kisiasa katika muungano wa Azimio la Umoja imezidi kusambaratisha muungano huo baada ya baraza kuu la chama cha DAP-K kutangaza kujiondoa katika muungano huo.

DAP-K ni moja ya vymaa anzu vilivyounda muungano huo kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 2022 wakishirikiana na ODM, Wiper, Jubilee miongoni mwa vyama vingine.

Katika mkutano uliofanyka mjini Webuye kaunti ya Bungoma, kinara wa chama hicho Eugene Wamalwa alitaja kusalitiwa na ODM kama moja ya sababu ya kujiondoa katika Azimio.

Wamalwa alishjtumu kinara wa ODM Raila Odinga kwa kushirikiana na serikali ya vKenya kwanza kupandisha ushuru, kupitisha miswada isiyofaa na hata kusababisha nchi kuwa katika vhali ngumu ya kiuchumi ambayo inawakandamiza wananchi wa chini.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Chama hicho pia kilionekana vkukashifu hatua ya rais William Ruto kumng’atua ofisini aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua.

DAP-K pia walitangaza kumuidhinisha Wamalwa kupeperusha bendera yao katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2027.

"DAP-K itasimamisha wagombeaji katika nyadhifa zote kuanzia MCA hadi Wabunge hadi Wawakilishi wa Wanawake hadi Ugavana hadi Seneta hadi Rais na wako kwa kweli wamepewa jukumu hilo kuu la kubeba bendera katika kinyang'anyiro cha urais Agosti 10, 2027."

"Tunasema kama DAP-K kwamba hatuwezi na hatuwezi tena kuona inafaa kuendelea kuwa na uhusiano na watu ambao hawana nia kama sisi tena, ambao wameendelea kumsaidia na kumsaidia Zakayo kurejesha kodi kali," Wamalwa alisema.

Wamalwa aidha alitaja ushirikiano wa baadhi ya viongozi wa muungano huo na Serikali tawala ya Kenya Kwanza ambao umefanya muungano huo kutopendwa na wananchi pamoja na kuunga mkono kuondolewa kwa Gachagua kuwa sababu nyingine za hatua hiyo kali.