Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru anasema mpango wa serikali wa nyumba za bei nafuu unaweza kusaidia kulinda ardhi ya kilimo isimezwa na maendeleo ya makaazi. Waiguru anasema kwamba kuweka nyumba katika maeneo yaliyotengwa kutaruhusu familia kuhifadhi ardhi ya kilimo huku ikiboresha upatikanaji wa huduma muhimu. Anataja Mwea, ambapo wakaazi wanaishi katika vituo vya mijini na husafiri kwenda mashambani mwao kulima, akisema mfumo huo unaweza kuigwa katika maeneo mengine ya kilimo.
ANNE WAIGURU – HOUSING