Kenya Police itakuwa mwenyeji wa AFC Leopards huko Nyayo huku pande zote mbili zikitafuta ushindi wao wa kwanza msimu huu baada ya kutoka sare katika mechi zao za ufunguzi dhidi ya Migori Youth na Bandari FC mtawalia. Nahodha wa Leopard, Kayci Odhiambo, anasema ni muhimu kwa timu hiyo kushinda mechi hiyo, ili kuhakikisha wanaendeleza matarajio yao ya ubingwa wa ligi. Ingwe ilimaliza ya pili juu kidogo ya Police FC msimu uliopita, na itakuwa ikitafuta ubingwa wao wa kwanza wa ligi katika miaka 19. Mechi hiyo itaanza saa kumi jioni.

Jua linashuhudiwa Makindu, Mtito a ndei na Voi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.