Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, amemshtumu Rais William Ruto kwa kuwaonyesha wakaazi wa kaunti hiyo kuwa kinyume na maendeleo huku kukiwa na mzozo kuhusu Soko la Masinde Muliro. Natembeya anasisitiza kwamba wafanyabiashara ambao tayari wamepewa vibanda sokoni wanapaswa kuruhusiwa kuendelea kufanya kazi bila kuingiliwa. Anasema wakazi wamefanya uamuzi wao, akiashiria kupinga kwake kuvurugika kwa shughuli za wafanyabiashara.

GEORGE NATEMBEYA – SOKO