Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amewasihi viongozi wa afya barani Afrika kuunga mkono ongezeko la ufadhili na mageuzi ili kuimarisha uwezo wa shirika hilo kuhudumia nchi wanachama. Akizungumza katika mkutano wa Kamati ya kikanda ya WHO, Tedros pia alitaka kuhitimishwa kwa mazungumzo kuhusu kiambatisho cha Upatikanaji na Ugawanaji wa Manufaa ya Vimelea ili kuwezesha kuridhiwa kwa Mkataba wa majanga. Alisema miezi kumi iliyobaki ilitoa fursa ya kuimarisha mageuzi na kuboresha ushirikiano wa afya duniani.
TEDROS GHEBREYESUS – HEALTH THREATS