Eldoret iko tayari kuandaa sherehe za Siku ya Mashujaa mwaka huu, huku Kamishna wa eneo la Bonde la Ufa Abdi Hassan akielezea jiji hilo kama ukumbi unaofaa kwa sababu ya urithi wake mkubwa wa michezo na mchango wake kwa mafanikio ya Kenya katika riadha. Hassan alisema tukio hilo litaonyesha mafanikio ya michezo ya eneo hilo na mchango wake katika maendeleo ya kitaifa, usalama na ukuaji wa uchumi. Wakati huo huo Katibu wa usalama Raymond Omollo anasema kila kitu kiko tayari kwa sherehe hizo.
RAYMONDO OMOLLO – CELEBRATIONS