Waziri wa usalama, Kipchumba Murkomen, amewahakikishia Wakenya usalama wa kutosha wakati wa sherehe za Siku ya Mashujaa zitakazofanyika kesho mjini Eldoret. Murkomen alisema maafisa wa usalama wamepelekwa katika eneo hilo ili kudumisha utulivu na kusimamia umati, huku akiwasihi wakaazi na wageni kuepuka msongamano mkubwa unaoweza kusababisha kukanyagana katika uwanja mkuu wa sherehe. Pia, aliwataka wale watakaohudhuria hafla hiyo ya kitaifa kushirikiana na waandaaji na kuwa waangalifu ili kuhakikisha sherehe hizo zinaendelea kwa usalama.