Tusker FC ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Singida Black Stars ya Tanzania katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho la CAF katika uwanja wa Nyayo jana. Baada ya kipindi cha kwanza kisichokuwa na bao, Jeancy Mboma alifunga bao dakika ya 52 na kuipa Singida faida muhimu. Pande zote mbili zilikosa fursa kadhaa mechi ilipomalizika kwa faida ya Singida. Brewers wanakabiliwa na kazi ngumu katika mechi ya marudiano, huku wakitafuta kupindua pungufu jijini Dar es Salaam wikendi ijayo.
Katika ligi kuu ya sportpesa, Murang'a Seal iliwashinda Posta Rangers 5-1 na kupata ushindi mkubwa zaidi katika mechi ya siku ya pili jana. Majaliwa Charo na Josphat Lopaga walifunga mabao mawili kila mmoja, huku Michael Macharia akiongeza moja kwa Seals. Wakati huo huo, Kakamega Homeboyz walipambana na kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Ulinzi Stars, huku Maurice Ojwang akifunga bao la kusawazisha la dakika za mwisho baada ya Jacob Onyango kufungua mabao katika kipindi cha kwanza. Katika Uwanja wa Afraha, Shabana FC ilitoka sare ya0-0 na Nairobi United.
Vipindi vya anga kavu vinashuhuiwa Kericho, Kitale na Kisii.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.