Noni Madueke alitoka benchi na kuipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya Nottingham katika ligi ya Primia hapo jana. Shambulio la Madueke dakika ya 80 lilikuwa shuti pekee la mshambuliaji huyo lililolenga lango na liliwarudisha hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 18, pointi tatu nyuma ya vinara Manchester City. Wakati huo huo, Brighton iliichapa Crystal Palace 5-0 na kurudi katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 18.

Mechi nyingine ya siku ya saba ilishuhudia Manchester United ikitoka sare ya 1-1 na Leeds. Calvert-lewin alifuta juhudi za Bryan Mbeumo katika kipindi cha kwanza na kuilaani United kwa sare yao ya tatu mfululizo na kuwaacha katika nafasi ya 13 kwenye jedwali la ligi kuu.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.