Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, ameeleza imani yake kamili katika uwezo wa kundi lake la kisiasa kupata uungwaji mkono kote nchini. Akizungumzia azma yake ya kuwania urais mwaka 2027, kiongozi huyo wa 'Linda Mwananchi' aliwajibu wakosoaji wanaotilia shaka uzoefu wake wa kisiasa na uwezo wake wa kifedha. Sifuna pia aliikosoa serikali kwa madai ya kuwakwamisha viongozi wa upinzani, akitolea mfano unyanyasaji dhidi ya Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya.
EDWIN SIFUNA – PRESIDENT