Vyama vya wafanyakazi wa sekta ya afya nchini vinatoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi wa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi vya Ebola na magonjwa mengine ya kuambukiza. Hii inafuatia uthibitisho kutoka kwa Wizara ya Afya kwamba wahudumu watatu wa afya ni miongoni mwa wale waliopimwa na kupatikana na virusi hivyo. Katibu Mkuu wa KMPDU, Davji Atella, anasema madaktari hawatahatarisha maisha yao ikiwa serikali itashindwa kutoa vifaa vya kutosha vya kujikinga binafsi.

DAVJI ATELLA - PROTECT