Mbunge wa Mwala, Vincent Kawaya, ametoa wito kwa Chama cha Wahadhiri UASU kuacha kuwatumia wanafunzi kuitishia serikali, na badala yake warejee kwenye meza ya mazungumzo ili kutatua mgomo wa wahadhiri unaoendelea. Ingawa anatambua haki za wahadhiri, Kawaya anabaini kuwa maelfu ya wanafunzi wanapoteza muda muhimu wa masomo. Mbunge huyo anahimiza pande zote mbili kuwa na subira na kurejesha hali ya kawaida ya masomo.
VINCENT KAWAYA – STRIKE