Chama cha Ustawi wa Wasafiri cha Kaunti kimeonya kuwa ongezeko la hivi karibuni la bei ya mafuta litasababisha kupanda kwa gharama ya maisha. Chama hicho kimeipa Mamlaka ya EPRA muda wa siku 14 kubatilisha uamuzi huo, kikidai kuwa ulifanywa bila kushirikisha umma au wadau wa sekta ya uchukuzi. Vilevile, kinaitaka Wizara ya Nishati kuingilia kati na kupunguza bei ya mafuta, huku ikitishia kuchukua hatua za kisheria iwapo matakwa yake hayatatekelezwa.

VOXPOP – COCOWA