Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, ametoa wito kwa NSSF na bodi yake ya wadhamini kupinga shinikizo la kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027, huku akikanusha madai ya baadhi ya wabunge kwamba wachangiaji wananyimwa pesa zao. Atwoli alisema madai hayo yanapuuza ukuaji mkubwa wa hazina hiyo, akibaini kuwa thamani ya uwekezaji wake imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 312 hadi Shilingi bilioni 814 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita..