Kocha Mkuu wa Tusker FC, Julien Mette, anasisitiza kuwa wachezaji wa klabu na wale wa timu ya taifa wanapaswa kuwa na imani ya kupata matokeo mazuri wakati wote, bila kujali ukubwa wa mpinzani. Kuelekea mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho la CAF siku ya Jumapili dhidi ya timu ya Tanzania, Singida, Mfaransa huyo anatarajia nyota wake kama Aboud Omar, Brian Bwire na wengine wenye uzoefu wa kimataifa kuonyesha kiwango cha juu. Timu ya Singida iliwasili nchini jana na itafanya mazoezi kesho katika uwanja utakaotumika kwa mechi hiyo, Uwanja wa Nyayo.

JULIEN METTE - SINGIDA

 

Aliyekuwa winga wa Manchester City, Riyad Mahrez, amejiunga na klabu ya Al Shamal SC ya Qatar kwa uhamisho huru. Mahrez alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Al Ahli mwezi Julai, klabu aliyoitumikia kwa miaka mitatu katika Ligi ya Saudi Arabia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliwakilisha Algeria katika Kombe la Dunia msimu huu wa joto, ambapo alihusika katika mabao matatu katika mechi nne, huku timu hiyo ikifika hatua ya 32 bora. Mahrez alijiunga na Al Ahli mwaka 2023 na kufanikiwa kushinda mataji ya Asian Champions League Elite katika miaka ya 2025 na 2026.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.