Serikali imeahidi kuharakisha miradi ya maendeleo katika Kaunti ya West Pokot ili kuboresha miundombinu na utoaji wa huduma. Rais William Ruto amesema serikali imetenga shilingi bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha mtandao wa barabara kote katika kaunti hiyo. Pia ametangaza mipango ya kujenga soko la kisasa katika mji wa Kapenguria, na kuwekeza shilingi bilioni 2.6 nyingine ili kuunganisha nyumba 10,000 za ziada na umeme.
WILLIAM RUTO-COUNTY