Rais William Ruto ameelezea mradi wa nyumba za bei nafuu kuwa ndiyo mpango wenye matokeo makubwa zaidi katika utawala wake. Akizungumza huko West Pokot, Ruto alisema kuwa mpango huo unawapa Wakenya makaazi bora, unaboresha hali ya maisha kwa wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi, na kuongeza nafasi za malazi kwa wanafunzi. Aliongeza kuwa mradi huo umetoa fursa za ajira kwa maelfu ya Wakenya.
WILLIAM RUTO-HOUSING