Rais William Ruto amemkosoa Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, kwa kupinga hatua ya serikali ya kutumia Ushuru wa Matengenezo ya Barabara kama dhamana ya kupata fedha. Akizungumza huko West Pokot, Ruto alisema serikali yake itaendelea kutenga fedha za kutosha ili kukuza ujenzi wa barabara kwa usawa kote nchini. Aliongeza kuwa West Pokot, eneo alilolielezea kuwa limekuwa likitengwa kimaendeleo kwa muda mrefu, litapewa kipaumbele kipya cha maendeleo chini ya utawala wake.
WILLIAM RUTO-ROADS