Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia maafisa wa usalama wa Serikali na ofisi zao kupanga vurugu, akisema vitendo vya kuvunja sheria havitavumiliwa. Akihutubia wakaazi wa Eldama Ravine, Murkomen alisema kwamba baadhi ya wanasiasa wanafurahia usalama wa Serikali lakini bado wanashiriki katika kupanga machafuko wakati wa mikutano ya kisiasa.

KIPCHUMBA MURKOMEN - JIRANI