Beki wa Manchester United, Lisandro Martinez, anasema alizungumza kwa hasira na ghadhabu alipotoa shutuma dhidi ya uongozi wa klabu hiyo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliikosoa United kwa kushindwa kuimarisha kikosi wakati wa majira ya joto, licha ya timu hiyo kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa. Kauli hizo alizitoa baada ya timu hiyo kupoteza 2-0 dhidi ya Atletico Madrid katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa. Martinez alisema alitarajia uwekezaji mkubwa zaidi katika kikosi cha United, pamoja na mchango zaidi kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi, Jason Wilcox.



Anfa kavu inashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.