Maelfu ya Wakenya wamekusanyika katika Uwanja wa Migwena, Siaya, kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya kumbukumbu ni pamoja na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, na Martha Karua. Mkusanyiko huo unawaleta pamoja viongozi na wafuasi ili kukumbuka urithi wa kisiasa wa Raila na kutafakari mchango wake katika safari ya kisiasa ya Kenya.
VOX POP – ANNIVERSARY