Chama cha Madaktari KMPDU kimesifu juhudi za Wizara ya Afya katika kuimarisha mikakati ya nchi ya kukabiliana na Ebola. Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu Dennis Miskellah amezikosoa serikali za kaunti kwa kushindwa kutoa bima ya matibabu kwa wahudumu wa afya. Amewatuhumu kwa kuachia jukumu la kudhibiti dharura kwa serikali ya kitaifa, huku wakidai kuwa na mamlaka juu ya bajeti, licha ya kwamba sekta ya afya kwa kiasi kikubwa imegatuliwa.


DENNIS MISKELLAH –EBOLA