Naibu Rais Kithure Kindiki anasema mapato yatokanayo na uuzaji wa viwanda vilivyotwaliwa kutoka kwa wazalishaji wa vitu vyenye madhara yatatumika kuanzisha vituo vya ukarabati. Kindiki alisema serikali imepanga kuwalenga wazalishaji wa kemikali hatari na bidhaa ghushi, ikiwa ni sehemu ya mkakati ulioboreshwa dhidi ya vitu haramu. Alisema serikali pia itawafuatilia wauzaji, wasambazaji, na magenge yanayojihusisha na biashara hiyo.


KITHURE KINDIKI - GOING