Kenya ilirekodi matukio ya vitisho vya mtandaoni bilioni 11.12 katika mwaka wa fedha uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 29 kutoka bilioni 8.62 katika mwaka uliotangulia. Takwimu hizo kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano ziliwasilishwa katika Mkutano wa Nne wa Usalama wa Mtandao wa Safaricom jijini Nairobi, ambao ulijikita katika kuimarisha usalama wa kidijitali huku kukiwa na ongezeko la vitisho vinavyotokana na AI, ikiwemo 'deepfakes', kujifanya mtu mwingine, ulaghai wa kiotomatiki, na programu hasidi za kudai fidia (ransomware).


PETER NDEGWA – THREATS