Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe ametoa wito wa mageuzi katika tasnia ya kahawa duniani ili kuwalinda wakulima, kuimarisha kanuni na kuhakikisha uzalishaji endelevu. Akizungumza katika Jukwaa la Kimataifa la Mikakati ya Kahawa la Italia, Kagwe alihimiza ushirikiano imara kati ya nchi zinazozalisha na zinazotumia kahawa ili kuongeza uzalishaji, kuboresha mapato ya wakulima na kupanua masoko. Akitoa mfano wa Kenya, alibaini kuwa uzalishaji wa kahawa umepungua kutoka takriban tani elfu 150 hadi elfu 50, akionya kwamba sera lazima zifanye kilimo cha kahawa kiwe cha ushindani.

MUTAHI KAGWE - CHOICE