Gavana wa Murang’a, Irungu Kang’ata, analalamikia kusitishwa kwa jukwaa la kidijitali la afya la kaunti hiyo, Afya.ke, akionya kuwa hatua hiyo inaweza kuvuruga huduma za afya na upatikanaji wa kumbukumbu za wagonjwa. Kang’ata anasema kuwa uamuzi wa kuhamishia vituo vya afya vya umma kwenye mfumo wa kitaifa wa 'Taifa Care' unakinzana na ahadi zilizotolewa awali na Waziri wa Afya, Aden Duale, kwamba mfumo wa Afya.ke ungeunganishwa na mfumo mwingine, na si kusitishwa.

IRUNGU KANG’ATA – SYSTEM